MISEMO KATIKA LUGHA ZA MAGARI: DIVAI MPYA?

Ahmad Kipacha
2014 SWAHILI FORUM   unpublished
misemo mipya imezuka bali hata ile misemo ya asili imepindwa na kutumiwa katika miktadha mipya. 1 Waandishi wa semi za magari ni madereva, utingo au wamiliki wa vyombo hivyo. 2 Tumebaini makundi matatu ya misemo katika data yetu, yaani misemo kongwe, misemo pindwa na misemo ibuka, kwa kuakisi nadharia za methali na misemo za Mieder & Litovkina (1999), Mieder (2007) na Litovkina (2011). Je, misemo hiyo ni mkondo wa fikra mpya za watu kama alivyotabiri Ke-zilahabi (1988, 1995)? Since the
more » ... Since the introduction of the private commercial motor transport services in Tanzania in the 1990s, the inscription of sayings has shifted from their mainly traditional platforms of female cotton wrap (Kanga), palm leaf food cover (kawa) or hand fan (kipepeo) onto the tailgate, sideboards or mudguards of commercial automobiles. The vehicle owners and/or their operators are inscribers of these automobile slogans. I analyse them in three forms: standard, parodied and innovated sayings adopting the paremiological approaches by Mieder & Litovkina (1999), Mieder (2007), Litovkina (2011). Do these forms of car inscriptions fulfill the prediction by Kezilahabi (1988, 1995) on the imminent transformation of the Swahili sayings to become a platform for negotiation of people's tumultuous life challenges and desires? Utangulizi Tanzania imepitia mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi tangu ipate uhuru kutoka kwa Waingereza. 3 Palikuwepo na jaribio la mfumo wa Ujamaa kati ya 1967 hadi 1985 na hivi sasa nchi imo katika mfumo wa soko huria. Hali hiyo ilibadilisha mfumo wa umiliki na utoaji huduma za usafiri ambapo sekta binafsi iliruhusiwa kushiriki kutoa huduma hizo kibiashara na hapo ndipo palipojitokeza fursa ya kumwagika kwa vyombo vya usafiri binafsi vinavyo jiendesha kibiashara mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kwa sasa tunashuhudia vijana wengi wakimiliki usafiri wa pikipiki za magurudumu mawili au matatu (bodaboda au bajaji) na kupanuka kwa sekta ya ujasiriamali unaoambatana na shughuli za vyombo vya moto ikiwemo gereji bubu, maduka ya spea za kuchinja, yadi za magari ya mitumba kutokea Japan, waosha magari nk. Idadi kubwa ya 1 Mada imehamasishwa na makala ya Reznikov (2009): Old Wine in New Bottles: Modern Russian Anti-proverbs. 2 Mara nyingi madereva na utingo si wamiliki wa vyombo vya usafiri wa kibiashara. Hata hivyo kunakuwa na maku-baliano ya kuandika misemo katika vyombo hivyo pengine kwa shinikizo la mwenye gari au matakwa ya waendeshaji katika muktadha mzima wa kibiashara. Baadhi ya misemo ni matukio halisi (metonomia) yaliyowa-tokea waandishi wa misemo hiyo. 3 Tanzania ni muungano wa nchi za Zanzibar na Tanganyika zilizoungana mwaka 1964. Utawala wa Julius Nyerere kama rais wa Tanzania ulidumu kati ya 1964 hadi 1985. Kipindi hicho kilitawaliwa na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, yenye kuweka njia zote kuu za uchumi pamoja na usafirishaji chini ya mashirika ya umma yaliyo si-mamiwa na serikali kuu.
fatcat:4scooo3e4bbohdrrna2zimyq74