Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda

Willy Wanyenya
2020 East African Journal of Swahili Studies  
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Kwa kurejelea jamii hii, mtafiti alieleza namna wazazi wanavyotumia lugha kulea watoto wao. Alifanya hivyo kwa kunukuu baadhi ya semi ambazo zinasemekana zinatumiwa na wazazi katika shughuli ya kulea watoto. Ni kweli kwamba lugha yoyote ile hufanya kazi nyingi sana kama vile kutumbuiza watu, kuficha
more » ... za watu, kuficha siri, kuseng'enya watu, kuibia watu, kutongozana, kushawishi, kugombana, kujitetea, kufundisha, nakadhalika. Hii ni kwa sababu bila kutumia lugha, mtu hawezi akaimba, akagombana, akaiba kwa kudang'anya, akafundisha, akaseng'enya, akatongoza, n.k. Hata hivyo, katika makala haya, mtafiti alijikita kwenye malezi ya watoto. Katika kazi hii, mtafiti alizingatia semi mbalimbali ambazo Wamasaaba huzitumia kwa ajili ya kuwaelekeza watoto wao ili wasije wakatenda maovu ukubwani. Katika jamii mbalimbali, watu hutumia lugha kutekeleza jambo hili. Jamii hasa zile za jadi zilitumia lugha kuwaelekeza watoto wao. Kuna namna ambavyo walisuka lugha kisanaa kwa lengo la kufunza watoto wao. Hii ni kwa sababu hawakuwa na madarasa maalumu mwa kufunzia watoto wao kama ilivyo sasa. Katika jamii hizo, shule zenyewe hazikuwepo. Kwa hiyo, lugha ndiyo ilikuwa chombo maalumu cha kufunzia watoto. Matumizi ya lugha yalidhamiria kukuza watoto wenye tabia nzuri. Hii ni kwa sababu watoto wenye tabia mbaya waliletea wazazi wao aibu. Hivyo basi, katika kazi hii, mtafiti alijikita katika matumizi ya lugha na kueleza jinsi Wamasaaba wanavyotumia semi mbalimbali kuelekeza watoto wao kitabia.
doi:10.37284/eajss.2.1.151 fatcat:s2or5nabu5hkrdbhoi2efcjhni